Tafuta

Njiwa ya amani Njiwa ya amani  (©adrenalinapura - stock.adobe.com)

"Pax et Bonum,"mkutano na maandamano na mishumaa kwa ajili ya amani na Kard.Pizzaballa

SDominika tarehe 8 Juni,mpango uliohamasishwa na Azione Cattolica na Taasisi ya Toniolo utaona fursa ya kuzungumzia hali ya kupokonya silaha na vita.Mzeituni utatolewa kwa Manispaa ya Roma katika kukumbuka mkutano katika bustani ya Vatican 2014,pamoja na Papa Francisko na marais wa Israel na Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina.

Vatican News  

Kama sehemu ya Jubilei ya Vyama, Harakati na Jumuiya Mpya itakayofanyika mwishoni mwa juma, Ijumaa tarehe 6 Juni 2025, utawasilishwa  mkutano na waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa "Pax et Bonum”: Kujenga Amani kwa Malengo ya Pamoja, kwenye Njia ya Sheria ya Kimataifa,  ukifuatiwa na Maandamano ya kwa mishumaa ili Kuomba Amani. Mipango hiyo, ambayo itafanyika Dominika alasiri, tarehe 8 Juni 2025 itaandaliwa na Jumuiya ya Kiitaliano ya matendo ya Kikatoliki, Jukwaa la Kimataifa la Matendo ya Kikatoliki (FIAC) na Taasisi ya Sheria ya Amani ya Kimataifa "Giuseppe Toniolo" na hafla ya "Dakika ya Amani" ambayo FIAC inapendekeza kila mwaka kwa  ajili ya kumbukumbu ya mkutano wa tarehe 8 Juni 2014, katika Mkutano kwenye Bustan za Vatican, kati ya rais wa Israel Shimon Peres na Mamlaka ya Palestina Abu Mazen, uliopendwa na Papa Francisko na mbele ya Patriaki wa Constantinople, Bartholomew I.

Sauti kutoka maeneo ya vita

Mkutano "Pax et Bonum" utaanza saa 11:30 jioni siku ya Dominika katika Ukumbi wa  Pio X, baada ya hotuba ya Kardinali Pierbattista Pizzaballa, Patriaki wa Yerusalemu ya Kilatini, kutakuwa na hotuba juu ya jukumu la sheria za kimataifa katika mgogoro wa kisiawa wa kimataifa na pia ushuhuda kutoka maeneo yenye migogoro kama vile  Ukraine, Burundi, Myanmar, Colombia na Nchi Takatifu. Maandamano  na mishumaa kwa ajili ya amani, itapitia katika njia ya  Conciliazione na kuishia Uwanja wa  Pia, kwa kuudhuriwa na meya wa Roma, Bwana Roberto Gualtieri, na katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo fungamani ya Kibinadamu, Kardinali Fabio Baggio.

Mzeituni kwa ajili ya  amani

Moja ya miti 12 ya mizeituni itakayopandwa katika ‘Villa Pamphili’ itawasilishwa kwa Manispaa ya Roma, pamoja na bamba la ukumbusho wa tukio hilo. Mpango wa kukumbuka mzeituni uliopandwa mwaka 2014 mjini Vatican. Katika mkutano na waandishi wa habari - taarifa kwa vyombo vya habari inasema - pendekezo la kuanzishwa kwa Wizara ya Amani litazinduliwa, ambalo litawasilishwa rasmi tarehe 24 Juni, 2025. Takwimu  kutoka katika Ripoti ya Uendelevu ya 2025 ya Chama cha Matendo Kikatoliki cha Italia, sasa katika toleo lake la saba, pia litawasilishwa. Picha ya kina ya huduma yake kwa Kanisa na nchi. Toleo hili linaangazia ushiriki na demokrasia, baada ya Juma la  Kijamii la Trieste na miaka 80 baada ya ukombozi kwa wanazi na wafashisti.

03 Juni 2025, 17:58