Tafuta

"León de Perú",Makala ya vyombo vya habari vya Vatican kuhusu miaka ya utume ya Prevost

Ratiba kati ya Chiclayo,Chulucanas,Callao,Lima,Trujillo,ili kugundua sura ya Papa Agostinian kupitia sauti na ushuhuda wa wale waliomfahamu,ambao walishirikiana naye au kupokea msaada wake kama mmisionari na mchungaji.Itakuja hivi karibuni kwenye chaneli za vyombo vya habari za Vatican.

Vatican News

Mmisionari, paroko, profesa, mwalimu, askofu, rafiki. Ni safari ya kuelekea Peru kwa kufuata nyayo za Robert Francis Prevost, ambaye sasa ni Papa Leo XIV, ambazo vyombo vya habari vya Vatican vinawasilisha huko León de Perú, filamu ya hali halisi inayounda upya miaka aliyotumikia katika nchi hiyo ya Amerika Kusini. Ni makala iliyoandaliwa na waandishi wa habari wa Radio Vatican, Vatican News: Salvatore Cernuzio, Felipe Herrera-Espaliat na Jaime Vizcaíno Haro, kazi hiyo inapitia maeneo ya Chulucanas, Trujillo, Lima, Callao, Chiclayo, ikigusa miji midogo na mikubwa, vijiji, wilaya, vitongoji, parokia, shule, nyumba za kitawa. Katika maeneo haya Padre wa wakati huo na Askofu Prevost ambayo alisherehekea, alihubiri, alifundisha, alifunza mambo ya kidini, alikutana na vijana, alisherehekea siku za kuzaliwa, walifanya kazi ya upendo katikati ya mikasa kama vile mafuriko ya El Niño na janga la Virusi vya uviko.

                           Robert Francis Prevost, giovane missionario in Perù

Robert Francis Prevost, kijana giovane mmissionari nchini Perù

Kazi ya kichungaji na kijamii ambayo historia nyingi za watu walioshirikiana na Papa wa baadaye na ambao walipokea kusikiliza na kupokea msaada kutoka kwake hunatoa mtazamo wa kweli. Ushuhuda wa maaskofu, kama vile wachungaji wa sasa wa Callao na Chulucanas, wa ndugu wa Shirika la  Mtakatifu Agostino au mapadre wa Parokia, kama vile Padre Cristophe Ntaganzwa, katika Wilaya maskini sana ya Pachacútec, walioathiriwa kwa nguvu na Uviko-19. Katika eneo hili msimamizi wa kitume wa wakati huo aliwasaidia watu bila kazi na kupunguza njaa kwa kupeleka chakula na dawa. Uingiliaji kati wa wakati unaofaa kama ule ambao kama Askofu wa Chiclayo, Prevost alitoa kwa idadi ya watu ambao mafuriko yalikuwa yamechukua kila kitu, akijitupa kwa ujasiri - kama Rocío, mmoja wa walionusurika, anavyosimulia - kwenye mitaa iliyofurika.

 

                         I parrocchiani di Santa Rita a Trujillo salutano "el padre Roberto"

Wanaparokia wa Mtakatifu Rita huko  Trujillo wakimsalimia "el padre Roberto"

Na tena, bado katika Chiclayo, ushuhuda wa Janina Sesa, mkurugenzi wa zamani wa Caritas, juu ya kampeni ya kuhakikisha oksijeni kwa wale walio katika dharura, au Berta, kupika katika moja ya comedores, jikoni la supu zilizowekwa katika Trujillo na "el padre Roberto" kulisha familia katika vitongoji. Kisha historia za ndani zaidi: kwa mfano, ile ya Sylvia, iliyookolewa na watawa kutoka kwa ulimwengu wa ukahaba ambao kwa ujasiri wake aliongoza Prevost kuanzisha Tume ya Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, au ile ya Hector na binti yake Mildred, ambaye Papa wa sasa ni Msimamizi wa Ubatizo.

Kila mmoja wa mashuhuda hawa anashirikisha jinsi walivyopitia jioni ya 'Habemus Papam' (yaani "Tunaye Papa") mnamo tarehe 8 Mei 2025 na kumtumia Papa ujumbe wa kibinafsi.

Makala hii ya León de Peru hivikaribuni itatangazwa kwenye idhaa rasmi za vyombo vya habari vya Vatican. Usikose kuifuatilia!

 

09 Juni 2025, 09:01