Papa Leo XIV,Maaskofu wa Madagascar:Ukaribu kwa watu wa Mungu ni ishara hai ya Injili.
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumatatu tarehe 16 Juni 2025 amekutana na Maaskofu wa Madagascar ambapo katika hotuba yake amefurahi kuwapokea katika kaburi la Mtume Petro, wao kama wachungaji wa Kanisa ambalo ni Madagascar waliofika Roma kwa hija ya Jubilei. Mkutano huo kwa Baba Mtakatifu una maana maalum, kwa sababu ni mkutano wake wa kwanza. Alimshukuru Bwana kwa fursa hiyo ya kidugu katika Kristo. Papa alisema kuwa alishangazwa kwa uamuzi wao wa kufika wote pamoja Roma, kama maaskofu wa Madagascar. Ni ishara nzuri ya umoja, iliyokuwa inapendwa tayari na mpendwa Hayati Papa Francisko ambaye alisema “tunamuhisi kiroho uwepo wake katika wakati huu.” Yeye alitembelea nchi yao kunako 2019 na miaka mitatu baadaye aliwapokea katika Ziara yao ya kichungaji (Visita ad Limina Apostolorum. Na kwa mara hii ni Jubiei, Mwaka wa neema uliotangazwa na Bwana Yesu ambaye aliwaita.
‘Ninyi ni mahujaji wa matumaini’
Baba Mtakatifu Leo XIV alisema kuwa ni vizuri kwamba wamegeuka kuwa wanahija wa matumaini, pamoja na mamiaelfu ya waamini ambao kila siku wanapita Mlango Mtakatifu wa Makanisa Makuu ya Kipapa. Awali ya yote wao ni wanahija wa matumaini wenyewe: wao ambao ni wachungaji, kama walivyokumbusha kuwa awali ya yote kondoo wa zizi, ambao Kristo anasema “mimi ni mlango wa kondoo.”(…) Ikiwa mtu anaingia kwa njia yangu, ataokoka; kuingia na kutoka na kupata malisho”(Yh 10,7.9). Na wakati huo huo wao wamegeuka kuwa mahujaji wa matumaini kwa ajili ya watu wao, kwa ajili ya familia, wazee, watoto, vijana, ili Makanisa ambayo ni ya Madagascar, kwa njia yao wapokee neema ya kutembea katika matumaini ambayo ni Yesu Kristo. Baba Mtakatifu Leo kadhalika alionesha furaha ya kuwasikiliza wakisimulia kwa furaha na majaribu ya kichungaji ambayo wanabeba kwa imani. Ukaribu wao kwa watu wa Mungu ni ishara hai ya Injili. Kwa njia hiyo aliwatia moyo kila mmoja katika huduma yake ya kiaskofu, kwa namna ya pekee ya kuwatunza mapadre ambao ni wahudumu wao wa kwanza na kaka zao walio karibu zaidi, ikiwa pamoja na watawa wa kike na kiume ambao wanajikita katika huduma.
Shukrani kwa uhai wa Kimisionari wa makanisa mahalia
Papa alitoa shukrani kwa ajili ya uhai wa kimisionari wa Makanisa yao mahalia, warithi wa ushuhuda wa watakatifu ambao, katika kuipeleka Injili katika nchi hiyo ya mbali, hawakuogopa kukataliwa wala kuteswa. Katika hao, Papa amependa kumbukumba Henri de Solages, Mmisionari wa kwanza ambaye hakukata tamaa ya kushindwa na gereza, Mtakatifu shahidi Jacques Berthieu ambaye damu yake ilikuwa mbegu ya kikristo nchini Madagascar.
Na damu yao iendelee kutia nguvu katika kujitolea wao binafsi kwa Kristo na kwa Kanisa lake, kati ya mafanikio na majaribu ya kichungaji ambayo wanapitia ili kufikia watu wa Mungu katika hali halisi za majimbo yao. Papa Leo XIV amewashauri wasitoe mtazamo wao kwa maskini; “wao ni kiini cha Injili na ni wapokeaji wa bahati ya kutangazwa kwa Habari Njema. Na mtambue ndani yao uso wa Kristo na tendo lenu la kichungaji daima lihuishwe na kuwajali sana watoto wadogo. Huduma yenu katika Jubile hii, zaidi ya majaribu, iwasaidie kuangazia upeo mpya wa matumaini unaotolewa na Kristo.”
Utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja
Kwa kufuata nyayo za Papa Francisko, Papa Leo XIV aliwaalika kutoa mazamo wa utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja na kuhifadhi uzuri wa Kisiwa kikubwa ambacho uzuri na udhaifu vimekabidhiwa kwao. Utunzaji wa nyumba yetu pamoja ni sehemu fungamani ya utume wao kinabii. Kwa hiyo watunze kazi ya uumbaji ambayo inalia na kuwafundisha waamini wao sanaa ya ulinzi na haki na amani. Kwa kihitimisha Papa Leo ameliwatia moyo wa kuendelea mbele katika huduma yao kwa ujasiri na matumaini. Mfuasi wa Mtume Peto anawasindika kwa sala zale na kwa upendo wake. Na Bikira Maria, Mama yetu wa Madagascar awalinde. Na Mwenyeheri Raphaël Rafiringa, Victoire Rasoamanarivo, Giacomo Berthieu na wtakatifu wpte wa nchi yao wawaombee. Papa Leo XIV aliwabariki kwa moyo.