Papa Leo akutana na Rais wa Bunge la Ulaya
Vatican News
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vyombo vya habari Vatican, Papa Leo XIV, Ijumaa tarehe 6 Juni 2025 alikutana katika Jumba la Kitume mjini Vatican, na Rais wa Bunge la Ulaya, Bwana António Costa, ambaye mara baada ya mkutano huo alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, akisindikizana na Monsinyo Mirosław Wachowski, Katibu Msaidizi wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na Mataisaha na Mashirika ya Kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, "katika mazungumzo yao, Srkretarieti ya Vatican walionesha uhusiano mwema kwa sehemu mbali mbali kati ya Vatican na Umoja wa Nchi za Ulaya na na shauku ya kuzidisha mijadala kuhusu masuala yenye maslahi kwa pamoja, hasa kuhusiana na pendekezo la kuanzisha mfuko wa kimataifa wa kuondoa njaa duniani na kukuza maendeleo ya nchi maskini zaidi. Katika muendelezo wa mazungumzo hayo, muktadha wa sasa wa kimataifa ulishughulikiwa, kwa kurejea juu ya migogoro ya Ukraine na Gaza."