Ukraine yaishambulia Urusi kwa ndege zisizo na rubani
Na Sarah Pelaji –Vatican.
Ukraine kwa mara nyingine tena imeishangaza Urusi na ulimwengu kwa shambulio hatari ambalo limefanyika kwa kutumia ndege zisizo na rubani dhidi ya viwanja vya ndege vya Urusi likiwa ni shambulio la kidhalimu na la kuthubutu. Wachambuzi wa masuala ya kijeshi wanasema ni shambulizi lililopangwa kwa uangalifu na kutekelezwa bila dosari. Vikundi vya makomando wa Ukraine vilijipenyeza katika eneo la adui na kufanya mashambulio tarehe 01 June 2025 kwa ndege nyingi zisizo na rubani zilizo na silaha dhidi ya vituo vinne vya anga ambapo sehemu ya meli ya Urusi ya mashambulizi ya kimkakati imewekwa.
"Urusi imepata hasara kubwa, ya haki na inayostahili," alisema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenksky, ambaye alihakikisha kwamba operesheni iliyofanywa na huduma zake za ujasusi "bila shaka itaishia kwenye vitabu vya historia."
Ndege 41 Urusi
Mwanablogu ya kijeshi wa Ukraine, Oleksandr Kovalenko alielezea ukubwa wa uharibifu uliotokea akisema kuwa, jeshi la anga la Urusi, katika hali yake ya sasa, halina uwezo wa kuzirejesha ndege hizo katika siku za usoni," aliandika kwenye chaneli yake ya Telegraph. Ukraine imeharibu ndege za kijeshi ambazo Moscow imekuwa ikitumia kuwatishia raia wa Ukraine kwa mashambulizi ya anga ya kila siku. Maafisa wa kijeshi wa Ukraine walisema ndege 41 za Urusi zilipigwa, zikiwemo za kimkakati za kushambulia na za uchunguzi, huku baadhi zikiharibiwa kabisa. Miongoni mwa ndege zilizoharibiwa ni Tupolev 95s (Tu-95s) na 22M3s. Kyiv pia inasema iliharibu Beriev A-50, ndege ya ufuatiliaji na ujasusi, na Tu-160 mbili. Kwa mujibu wa Justin Bronk, mtafiti mkuu katika Taasisi ya Royal United Services huko London, alisema shambulio hilo limekuwa "mafanikio ya kushangaza kwa operesheni maalum za Ukraine."
Kurejeshwa kwa eneo la Kursk
Iwapo itathibitishwa kuwa jumla ya ndege 41 za Urusi zimeharibiwa, itakuwa na athari kubwa kwa Kikosi cha Usafiri wa Anga wamasafa marefu wa Urusi. Haya yanatokea baada ya miezi kadhaa nyuma Rais Vladimir V. Putin wa Urusi alipokuwa akionesha na kuthibitisha kuwa majeshi yake yako karibu kushinda vita nchini Ukraine. Alidokeza kuwa hana sababu yoyote ya kukubali kusitisha mapigano, kwa kuwa majeshi ya Urusi yako tayari kuendelea kupigana hadi mwisho. Alipongeza kurejeshwa kwa eneo la magharibi la Kursk kutoka kwa Ukraine akisema kwamba, linapokuja suala la wanajeshi wa Ukraine, Moscow inaamini kuwa tayari wameshamaliza kuwakabili. Hata hivyo Kyiv ilitoa majibu yake tarehe 1 June 2025 kwa kuishambulia Urusi.